Jumlisha kutoka 1 mpaka 100 - IchigoJam

Kutumia "?", Uliza kompyuta "1+1".
?1+1
Ilijibu "2" kwa kibonye ENTER. Hivyo basi, vipi kuhusu "1+2"?
?1+2
Je, kuna 'bowling pins' ngapi jumla?
?1+2+3+4
Ziko 'pins' 10.
Nini kitatokea kama itaongezeka kwa safuwima 'column' 1?
Tumia kibonye kishale cha juu/kushoto/kulia, inarejeleza programu!
Chapa "+5" ili kujumlisha, na bonyeza kibonye ENTER.
?1+2+3+4+5
Yatakuwaje matokeo wakati wa kujumlisha 1 kwa 10 kama hivi? Kujumlisha 1 kwa 10 katika mwendo huu, jibu ni ngapi?
?1+2+3+4+5+6+7+8+9+10
Vipi kama ni kujumlisha kutoka 1 mpaka 100, inaonekana kuwa gumu!?.
Hivyo tumia komandi ya kurudia, "FOR".
FOR I=1 TO 100:?I:NEXT
Andaa muundo-wa-herufi "A", itakayoweza kujumlishwa zaidi na zaidi.
A=0 OK FOR I=1 TO 100:A=A+I:NEXT OK ?A 5050
Jaribu sasa!
1. Yapi matokeo kwa kujumlisha toka 1 mpaka 12?
2. Yapi matokeo kwa kujumlisha toka 1 mpaka 20?
3. Yapi matokeo kwa kujumlisha toka 1 mpaka 200?
4. Yapi matokeo kwa kujumlisha toka 1 mpaka 300?
5. Ipi namba ya kikomo ambayo inaweza kukokotolewa kwa uzuri?
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp