Tengenza namba jozi / BIN$

Kuna namba, silabi, alfabeti, vibambo mbalimbali, lakini kibambo kinachotumika na kompyuta ni "0" na "1" tu.

Kwa kawaida, kama ukijumlisha 1 katika 9, itakuwa 10 na vibambo 2, lakini kwasababu kuna 0 na 1 tu, moja pekee itajumlishwa kwa 1, hivyo itakuwa 10(moja sifuri) na vibambo 2. Hii ni namba jozi.

"BIN$" ni komandi inayobadili namba kuwa namba jozi.

?BIN$(2) 10 ?BIN$(10) 1010
Alama "` "(kibonye SHIFT + "@" au kushoto kwa "1") inabadili namba jozi kuwa namba.
?`1111 15 ?`100000000 256
0, 1, 2, 3, 4 ... ihesabu kwa namba jozi.
FOR I=0 TO 256:?BIN$(I),I:WAIT 30:NEXT 0 0 1 1 10 2 11 3
Namba jozi zinahesabu kwa biti "bit".
3 ni biti 2 zenye "11", 8 ni biti 4 zenye "1000".
Jaribu sasa!
1. Hebu fanya "16" kuwa namba jozi
2. Hebu fanya namba jozi "101", "1010", "10100" kuwa namba
3. Hebu fanya "40" kuwa namba jozi
4. Ni namba gani ya kiwango cha juu ambayo inaweza kuwakilishwa na biti 5?
5. Hebu fanya "-1" kuwa namba jozi
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp