Julisha mawazo / BTN

Hebu iambie kompyuta mawazo yako kwa kutumia kitufe cha upande wa kushoto katika IchigoJam.
?BTN()
Kama ukibonyeza kibonye ENTER bila kubonyeza kitufe, itaonyesha sifuri (0). Bonyeza kishale cha juu mara tatu kilicho kwa chini kulia katika kibodi, sogeza kishale cha mraba kinachopepesa, halafu shindilia chini kitufe katika ichigojam na bonyeza kibonye ENTER.
Ni mafanikio kama itaonyesha "1"!
Rudia kwa kutumia komandi ya "GOTO".
10 ?BTN() 20 GOTO 10 RUN
"0" itaonyesha katika safu, hebu tujaribu kubonyeza au kuachia kitufe.
Kuisimamisha, tumia kibonye ESC(Escape).
Programu ambayo LED inawaka endapo kitufe kitabonyezwa.
10 LED BTN() 20 GOTO 10
Pia unaweza kutumia kibonye F5 badala ya komandi ya "RUN"!
Komandi ya "LED" itawasha endapo ni 1 na itapotea endapo ni 0, hivyo inawaka shanjari na kitufe kinavyobonyezwa.
Simamisha kwa kibonye ESC(Escape).
Ukibonyeza kitufe, ikonyeze haraka!
10 LED 1:WAIT 10-BTN()*5 20 LED 0:WAIT 10-BTN()*5 30 GOTO 10
"WAIT" ni komandi ya kusubiri.
Wakati ambapo kitufe hakijabonyezwa, ni "WAIT 10".
Kama kikibonyezwa, BTN() itakuwa 1, toa namba inayozidishwa na 5 kwa "* 5", hivyo inakuwa "WAIT 5".
Rudi nyuma katika mstari wa 10 kwa "GOTO", rudia.
Jaribu sasa!
1. Hebu tufanye ipepese kwa haraka zaidi, endapo kitufe kitabonyezwa.
2. Hebu tufanye ipepese taratibu, endapo kitufe kitabonyezwa.
3. Hebu tuiumbe upya iweze kuwasha wakati wote, endapo kitufe kitabonyezwa.
4. Hebu tuiumbe upya isiweze kuwasha kabisa, endapo kitufe hakitabonyezwa.
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp