Tengeneza ishara ya usiku / GOTO

Ishara yenye kupepesa kwa ajili ya usiku, inawaka na kuzima kila sekunde 0.5.
10 LED1:WAIT30:LED0:WAIT30 20 LED1:WAIT30:LED0:WAIT30 RUN
Chapa mstari wa 10 na bonyeza kibonye ENTER, kisha rejesha kielekezi mstari wa 10 na badili kiongozo "10" kuwa "20", na bonyeza kibonye ENTER.
Hakiki kama mstari wa 10 umenakiliwa katika mstari wa 20 kwa kutumia "LIST"!
Pepesa muda wote kwa "GOTO". Takribani mara 30,000 mpaka kunakucha.
10 LED1:WAIT30:LED0:WAIT30 20 GOTO 10
Namba iliyo baada ya "GOTO" inatoa muelekeo wa fikio.
> mstari wa 10, pepesa mara moja
> mstari 20, rukia mstari wa 10
Kuisimamisha, bonyeza kibonye [ESC].
Pepesa kwa haraka
LIST 10 LED1:WAIT3:LED0:WAIT3
Tengeneza mstari wa 15 kati ya mstari wa 10 na wa 20, kwa kubadilisha kiongozo "10" kuwa 15 na wait3 kuwa wait30, bonyeza kibonye ENTER. Onyesha programu kwa "LIST"(ama kibonye =F4), na kisha tekeleza kwa "RUN"(ama kibonye =F5).
15 LED1:WAIT30:LED0:WAIT30
Rudia kwa kubadilishana kati ya pepesa fupi na pepesa refu.
Jaribu sasa!
1. Hebu turejee katika programu ya ishara ya usiku
2. Refusha muda wa kuwaka pekee
3. Jaribu kuitengeneza iwe mchezo wa kupepesa kwa kasi na isimame ambapo inawaka
4. Tengeneza mistari ya namba, kuanzia 100 kwa hatua 100 m.f. 100,200,300
5. Hebu tutengeneze ruwaza ya kupepesa yenye kuvutia, na ringishia kwa yoyote.
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp