Iache iamue / IF

"IF" ni komandi ya kuacha kompyuta iamue.
10 IF BTN()=0 GOTO 10 RUN
kama kitufe hakijabonyezwa, mstari wa 10 utajirudia.
Pale utakapokibonyeza kitufe, programu itaenda kwa unaofuata, na kumalizika.
Kila wakati bonyeza kitufe, LED iwake na kuzima.
10 IF BTN()=0 GOTO 10 20 LED1 30 IF BTN()=0 GOTO 30 40 LED0 50 GOTO 10
Oh, wakati unabonyeza kitufe, LED inawaka?
Kwa kuwa kompyuta ina kasi, unapobonyeza kitufe itawasha LED na kusogea katika maamuzi mengine maramoja.
Ili isiende katika maamuzi mengine maramoja, ongezea subiri "WAIT".
10 IF BTN()=0 GOTO 10 20 LED1:WAIT30 30 IF BTN()=0 GOTO 30 40 LED0:WAIT30 50 GOTO 10
Jaribu sasa!
1. Endelea tu kubonyeza kitufe
2. Jaribu kubadili "WAIT30" kuwa "WAIT60"
3. Jaribu kubadili "WAIT30" kuwa "WAIT5"
4. Jaribu kubadili "IF BTN()=1"
5. Tengeneza programu ambayo kitufe kitapobonyezwa itaanza kupepesa LED
6. Tengeneza programu ambayo itaendesha LED katika hali ya kufurahisha
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp