Jibu katika namba / INPUT

Programu ambayo inatatua hesabu mbalimbali za kujumlisha kutumia "RND"(random).
Tumia "LET" kuhifadhi namba katika A mpaka Z.
10 LET A,RND(10) 20 LET B,RND(10) 30 ?A;"+";B RUN
Hebu dabiri ("RUN") mara kadhaa!
Ili kuhifadhi namba kwa kutumia kibodi, tumia komandi ya "INPUT".
40 INPUT C 50 ?C RUN
Mbele ya "?", chapa namba kwa kibodi na bonyeza kibonye ENTER.
Namba iliyowekwa katika C itahifadhiwa!
Kwa kuangalia majibu, "IF" inatumika kuamua.
60 IF C=A+B ?"SAWA"
Hebu tumia "ELSE" pale unapotaka kuonyesha makosa.
60 IF C=A+B ?"SAWA" ELSE ?"SI SAWA"
Pia inaweza kujitokeza ikiwa na swali kimaandishi.
40 INPUT "JIBU NI?",C
Jaribu sasa!
1. Hebu iunde upya iwe ya kujumlisha namba yenye tarakimu mbili.
2. Hebu iunde upya iwe hesabu rahisi mno
3. Hebu iunde upya iwe hesabu ya kuzidisha
4. Hebu pima muda wa kujibu kwa kutumia "TICK"
5. Hebu tengeneza mchezo wa kugonga namba
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp