Mchezo wa Mkono (Janken)

Mchezo wa mkono (maarufu kama Rock-Paper-Scissor) ni mchezo unaotumika haswa kuchagua bila upendeleo baina ya timu fulani.Kwa kutumia mkono kuna ishara tatu rock(jiwe), paper(karatasi) na scissors(mkasi)
- Gu: (rock) ni kukunja ngumi. (Gu inamshinda Choki)
- Choki: (scissors) tumia vidole viwili, igiza umbo la mkasi. (scissors inamshinda Pa)
- Pa: (paper) nyosha chini kiganja chako. (Pa inamshinda Gu)

Tumia komandi ya "Random" yenye namba 3 kama unataka kuamua Gu, Choki au Pa kwa kompyuta yako.
?RND(3)
Kwa mfano 0 inamaanisha Gu, 1 inamaanisha Choki, 2 inamaanisha Pa.
10 LET A,RND(3) 20 IF A=0 ?"GU" 30 IF A=1 ?"CHOKI" 40 IF A=2 ?"PA" RUN
Jaribu kuchapa RUN au bonyeza kibonye F5 kwa kurudia rudia!
Bonyeza kibonye F5 na sema alama ya mkono wako ili kushindana baada ya kutamka "Jan ken"!
Jaribu kuamua kwa kompyuta.
15 INPUT "YOUR HAND?",B 16 IF B=0 ?"GU - "; 17 IF B=1 ?"CHOKI - "; 18 IF B=2 ?"PA - "; 50 IF A=B ?"DRAW" 60 IF A-B=1 OR B-A=2 ?"WON!" 70 IF B-A=1 OR A-B=2 ?"LOST!"
Jaribu sasa!
1. Jaribu kushindana na programu katika kompyuta ya rafiki yako!
2. Jaribu kuumba kompyuta dhaifu kabisa!
3. Jaribu kuumba mchezo wa Janken wenye wachezaji 3, wewe na kompyuta 2!
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp