Mchezo wa Kawakudari

"Mchezo wa Kawakudari" ni mchezo ambao unaepa vizuizi na kutembea katika mto.
Kwanza, amua kibambo chako mwenyewe.
10 CLS:X=15 20 LC X,5:?"O" RUN
※Kwa 「"」, shikilia kibonye Shift na bonyeza 「'」. Kwa 「?」, shikilia kibonye Shift na bonyeza 「/」. Wakati mwingine maeneo haya yanaweza kubadilika kutegemeana na aina ya kibodi.
Kibambo cha adui, kujitokeza.
30 LC RND(32),23:?"*"
※ Kwa 「(」「)」, shikilia kibonye Shift na bonyeza 「8」「9」.
Hebu bonyeza kibonye F5(sawa kama "RUN") mara nyingi.
Rudia katika programu.
40 GOTO 20
Inakwenda kasi sana? Simamisha kwa kibonye ESCAPE, na ingiza "WAIT".
35 WAIT 3
Kuweza kusogea kwa kibonye mshale cha kushoto na/au kulia .
36 X=X-BTN(28)+BTN(29)
Pachika maamuzi ya kugonga ili kumalizika kwa mchezo!
37 IF SCR(X,5) END
Kama hujagongwa, mchezo unaendelea.
Jaribu sasa!
1. Hebu rekebisha mwendo
2. Hebu badili kuwa kibambo chako mwenyewe (shikilia kibonye ALT na bonyeza moja kati ya A mpaka V)
3. Hebu tuongeze vizuizi(mf. "***")
4. Hebu tufikiri kuhusu hadithi ya mchezo
5. Hebu tafuta vidokezo/ujanja(virusi)
6. Hebu fikiri jinsi ya kufuta kirusi
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp