Washa! / LED

Washa swichi ya IchigoJam. Chapa "LED1" katika kibodi yako. Bonyeza kibonye ENTER. (Kibonye ENTER kiko upande wa kulia na ni kikubwa)
LED1
Ni sawasawa endapo LED ya IchigoJam iliwaka na ukapata ujumbe "OK".
Chapa "LED0" ili kuzima.
LED0
Kibonye SPACE ni kikubwa na kiko katikati, kwa chini katika kibodi.
Type "LED 1" and the press ENTER key.
LED 1
Ni sawa vyovyote vile, nafasi ikiwepo au la.
Hebu chapa "RED0" na bonyeza kibonye ENTER.
RED0
LED haitazimika, utapata ujumbe "Syntax error".
Usihofu kuhusu kufanya makosa mara kwa mara! kompyuta haikasiriki kamwe.
Hebu chapa "ABD" bila kubonyeza kibonye ENTER.
ABD
Mara moja bonyeza kibonye Backspace.
Kibonye Backspace kiko juu upande wa kulia katika kibodi.
AB
Unaweza kufuta kibambo (character)! Hivyo usifofu kuhusu kukosea kuchapa.
Jaribu sasa!
1. Chapa "ABCDEFG"
2. Jaribu kuzima LED
3. Jaribu kuizima na kuiwasha kwa haraka
4. Chapa "BEEP" na bonyeza kibonye ENTER
5. Chapa "CLS" na bonyeza kibonye ENTER
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/en/ IchigoJam®jig.jp