Endesha mahali au sehemu / LOCATE

Hebu onyesha katika sehemu iliyoamuliwa!
Tumia "LOCATE" kuamua sehemu.
LOCATE 16,12:PRINT "*"
Bonyeza kibonye ENTER, '*' itaonyeshwa karibia na katikati.
Inamaanisha kwamba '*' itaonyeshwa katika nafasi ya 16 tokea upande wa kushoto, na nafasi ya 12 tokea upande wa juu.
Hebu tuonyeshe katika sehemu ya tofauti.
LOCATE 25,5:PRINT "*"
Badili namba katika "LOCATE", eneo la uonyesho litabadilika.
Kwa kweli, unaweza kutumia "LC" kama kifupisho cha "LOCATE".
LC 16,14:PRINT "*"
Pia vibambo vinaweza kuonyeshwa katika sehemu mbili tofauti.
LC 16,12:PRINT "@":LC 10,10:PRINT "*"
Pia jibu lililokokotolewa linaweza kuonyeshwa.
LC 16,14:PRINT 2+3
Unapotaka kufuta monita, bonyeza kibonye F1 au "CLS".
CLS
Jaribu sasa!
1. Onyesha "IchigoJam" katika 20 tokea kushoto na 10 tokea upande wa juu
2. Onyesha '@' katika sehemu mbili tofauti, yaani, katika 10 tokea upande wa kushoto, 17 tokea upande wa juu, na katika 25 tokea upande wa kushoto, 18 tokea upande wa juu
3. Onyesha matokeo ya "10-5" katika 15 tokea upande wa kushoto, 24 tokea upande wa juu
4. Onyesha kibambo ukipendacho katika sehemu uipendayo
5. Onyesha matokeo ya mahesabu uyapendayo katika sehemu uipendayo
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp