1 + 1 = 1, Fumbo la Mantiki

Tuna 0 na 1 tu (katika ulimwengu wa mantiki), sasa tufanye ukokotozi. Mosi tunaanza na kujumlisha. "|" (mwambaa wima).
?1|0 1 ?0|0 0 ?1|1 1
Hakuna ongezeko la tarakimu kwa kujumlisha 1 na 1, bado inabakia kuwa 1, hiyo ni "jumla ya mantiki".
Ifuatayo ni kuzidisha, tumia "&". (Tumia koma kutenganisha na kukokotoa kwa ujumla)
?1&1,0&1,1&0,0&0 1 0 0 0
Kama namba itazidishwa kwa 1, jibu litakuwa namba hiyo hiyo, na litakuwa 0 endapo itazidishwa kwa 0, Hiyo ni "kuzidisha ya mantiki".
Ili kujumlisha isivyo kawaida tumia "^". Hata kama namba zote mbili ni 1, jibu ni sifuri
?1^1,0^1,1^0,0^0 0 1 1 0 ?1|1,0|1,1|0,0|0 1 1 1 0
Ni pekee kwa 1^1, ila kwa nyinginezo zinabakia kuwa hivyo hivyo kama kwenye "jumla ya mantiki". Hiyo ni "XOR" (exclusive OR)
Ukokotozi wa mantiki unaweza kupangwa kwa ujumla hadi kufikia 16 (nambari ya juu zaidi)!
?BIN$(`1010|`0011,4) 1011
Kujumlisha namba jozi zenye tarakimu nne. Unaweza kukokotoa 1|0, 0|0, 1|1, 0|1 zote kwa mara moja!
Jaribu sasa!
1. Nini jawabu kwa 3|1?
2. Tumia kidokezo: ?BIN$(1),BIN$(2),BIN$(3), tatua fumbo 3|1
3. Hebu tufanye ukokotozi wa ?8323^35 na ?8323^35^35
4. Badili kuwa namba tofauti, hebu tucheze na namba za siri kwa kutumia mantiki
5. Hebu tufanye ukokotozi mbalimbali, tufanye mafumbo ya Mantiki

CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp