Hebu tufanye kadirio la juu!
49 ni 50, 45 ni 50, 44 & 41 pia ni 50, 40 ni 40.
Inaitwa kukadiria juu nafasi ya kwanza.
?44/10*10+10
50
Baada ya kukadiria chini, unaweza kuikadiria juu kwa kujumlishia 10!.
?40/10*10+10
50
Oh safi, 40 imebadilika na kuwa 50. Hebu amua kwa nafasi ya kwanza "ones place".
10 INPUT N
20 LET M,N%10
30 ?M
"%" ni alama ya kukokotoa baki katika ulimwengu wa IchigoJam BASIC.
Kama nafasi ya kwanza ni 0, ikadirie chini, na kama ni 1 au zaidi ikadirie juu.
40 IF M=0 ?N/10*10
50 IF M>=1 ?N/10*10+10