Tengeneza kibambo asili / PCG

"Kinyau" kitajitokeza kama utashikilia kibonye ALT cha kushoto katika kibodi na kubonyeza "C".
?CHR$(236)
Msimbo wa kibambo wa "kinyau" ni 236.
Ili kubadili hiki "kinyau" kuwa "fimbo".
POKE 236*8,8,8,8,8,8,8,8,8
Imebadilika!?
Sasa ni muda wa kubadili kuwa kimpira kidogo.
POKE 236*8,0,0,0,24,24,0,0,0
Kuwa mstari mshazari!
POKE 236*8,1,2,4,8,16,32,64,128
Programu ya kuandika mchoro uupendao kwa kutumia namba jozi, 0 na 1.
10 POKE236*8+0,`01111110 11 POKE236*8+1,`11011011 12 POKE236*8+2,`11111111 13 POKE236*8+3,`11000011 14 POKE236*8+4,`11111111 15 POKE236*8+5,`11111111 16 POKE236*8+6,`00011000 17 POKE236*8+7,`00011000 RUN
Bwana barafu anatokea!
Kurudi kwa "kinyau", tumia "CLP" (kifuta ruwaza).
CLP
Jaribu sasa!
1. Hebu tengeneza alama ya moyo
2. Hebu tengeneza kibambo ukipendacho
3. Hebu tuandike upya viumbe vigeni katika ALT + D kwa kubadili 236 kuwa 237 (masafa ya msimbo wa kibambo ni 224-255!)
4. Hebu tuonyeshe namba kwa ajili ya namba jozi "10000000"
5. Hebu tutengeneze msimbo wa kibambo asili kwa programu ya mstari mmoja .
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp