Tunga muziki / PLAY

Hakikisha miguu ya saketi ya sauti imechomekwa katika SOUND(SND) na GND kwenye IchigoJam yako.
PLAY"CDE"
Je umesikia sauti Do-re-mi?
Toni za Do-re-mi-fa-so-la-ti zinawakilishwa na CDEFGAB
PLAY"CDEFGAB"
Oktavo (=kiwango cha sauti) inaweza kubadilishwa kwa kutumia alfabeti "O" ikifuatiwa na namba.
PLAY"O4 CDEFGAB O5 C"
Unaweza kubadili urefu wa toni kwa kuweka namba.
PLAY"CDE2"
"2" katika "CDE2" inamaanisha nusu noti (half note). Mpangilio wa chaguo-msingi (bila namba) ni robo noti. Kwa kuweka "8" inamaanisha noti ya nane ambayo urefu wa toni yake ni nusu ya robo noti. "1" ina maana ya noti nzima.
"#" (sharp) Ni kuongeza toni kwa nusu toni, "-" (toa) ni kupunguza toni kwa nusu toni.
PLAY"C C# F-"
"R" inamaanisha unyamavu. Unaweza kubadili urefu wa unyamavu wa toni kwa kuweka namba baada ya R mfano "R2".
PLAY"CRC"
"T" inamaanisha kuiaandaa tempo. Mpangilio wa chaguo-msingi ni "T120" ikimaanisha robo noti 120 kwa sekunde.
PLAY"T240 CDE2 CDE2 GEDCDED2"
Hebu tujaribu!
1. Tengeneza muziki "Tulip" "Twinkle-Twinkle" "Old-MacDonald"
2. Chapa "PLAY" tu wakati wa kucheza muziki
3. Tengeneza muziki "wimbo wa Froggie"
4. Hebu tucheze kwa pamoja kama okestra na marafiki zako!
5. Hebu tunga muziki kutoka katika kitabu chako cha muziki!
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp