Kokotoa namba / PRINT

Hebu ipe swali kompyuta ambayo iko vizuri katika kukokotoa
Tumia "PRINT" kuonyesha ile iliyoainishwa.
PRINT 1+1
Bonyeza kibonye ENTER, mara-moja unaweza kupata jibu 「2」.
PRINT 15-7
Pia inawezekana kutoa.!
Katika kompyuta, alama ya kuzidisha inawakilishwa na kinyota '*'.
PRINT 3*5
Kugawanya ni mkwaju '/'. (namba ya juu ya sehemu:kushoto , namba ya chini ya sehemu:kulia)
PRINT 10/2
Kwa kweli, badala ya "PRINT" unaweza kutumia '?'.
?10/3
Oh!! Jibu ni la Uongo?
Ni jibu sahili katika "IchigoJam" ambayo haitumii desimali.
Baki inakokotolewa kwa kutumia '%'.
?10%3
Kwa sababu 10 gawanya kwa 3 ni 3 na baki ni 1, '1' itaonyeshwa.
Hatimaye, hebu tukokotoe namba kubwa.
?1000*100
Oh, jibu ni la ajabu!.
Kwa kweli, masafa ambayo IchigoJam inaweza kukokotoa yanaamuliwa kutoka -32768 mpaka 32767.
Jaribu sasa!
1. Hebu tutengeneze hesabu "100 + 200" katika IchigoJam
2. Hebu tutengeneze hesabu "8 * 7" katika IchigoJam
3. Hebu tutengeneze hesabu "100 / 25" katika IchigoJam
4. Hebu tukokotoe baki ya "30/8" kwa IchigoJam
5. Hebu tukokotoe 100,000,000 (10,000 * 10,000) kwa IchigoJam
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp