Tengeneza kete au dadu / RND (RANDOM)

Hebu tutengeneza kete mbalimbali!
?RND(3)
Namba ya aina gani imejitokeza?
RND (random) ni kete ambayo kuna nyuso zenye idadi sawa na namba iliyo katika mabano.
Chapa tena na bonyeza kibonye ENTER!
?RND(3)
Je namba iliyoonyeshwa imebadilika kulinganisha na mwanzo?
Oh! Lakini 3 haikutokea?
Hii inamaanisha kwamba namba tatu na 0 ikijumuishwa zitatokea.
Kama namba katika mabano ni 3, Ni namba 3 ambazo ni 0, 1, 2.
?RND(5)
Unaweza pia kubadili namba iliyo katika mabano.
Unataka kuiondoa 0?
Unataka kufanya namba ndogo kabisa kuwa ni 1 katika namba itakayotokea?
Katika jambo kama hilo ...
?RND(3)+1
Hii ni SAWA!
Kwa kuongeza 1 katika 0 ambayo ndio ilikuwa namba ndogo zaidi, namba ndogo zaidi katika namba itakayotokea inakuwa 1.
?RND(3)+3
Inaweza pia kubadili namba ndogo zaidi kati ya namba zitakazotokea.
Jaribu sasa!
1. Hebu tuonyeshe kwa nasibu namba yoyote kutoka 0 mpaka 6
2. Hebu tuonyeshe kwa nasibu namba yoyote kutoka 1 mpaka 6
3. Hebu tuonyeshe kwa nasibu namba yoyote kutoka 10 mpaka 20
4. Hebu tutengeneze kete ambayo itatoa namba uipendayo
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp