Kumbumbu ya programu / RUN/LIST

Hebu tujaribu kuhifadhi ruwaza ya kupepesa ya LED.
10 LED1:WAIT10
Kwa kuanza na namba, katika komandi inamaanisha "kuhifadhi".
Lakini LED haijawaka.
Komandi ya kudabiri ni "RUN" na kibonye ENTER, LED itawaka.
RUN
Inayofuata inaanza na 20, na ongeza kumbukumbu kwa kibonye ENTER.
20 LED0:WAIT10
Tumia "RUN" kudabiri programu iliyohifadhiwa.
Washa tena kwa "RUN"!
Ita kumbukumbu kwa "LIST".
LIST 10 LED1:WAIT10 20 LED0:WAIT10
Kupachika "WAIT" kati ya mstari wa 10 na 20.
15 WAIT50
Hakiki kwa "LIST", tekeleza kwa "RUN"!
Programu zenye namba za kufanana zitapandana (overwritten).
(Hakiki kwa "LIST"!)
15 WAIT110
Chapa namba pekee na bonyeza ENTER, itaufuta mstari ule.
15 LIST
Jaribu sasa!
1. Tumia kibonye F5 badala ya komandi ya "RUN"
2. Tumia kibonye F4 badala ya "LIST"
3. Hebu tutengeneze program itakayowasha LED mara mbili
4. Hebu tutengeneze programu itakayowasha LED kwa ruwaza ya kuvutia
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp