Tunza programu / SAVE/LOAD/NEW

Ni programu ya kuwasha LED. Tunza programu kwa kutumia "SAVE".
SAVE0 Saved 30byte OK
Endapo uwezo na "OK" vitaonyeshwa, kuhifadhi programu kumemalizika.
IchigoJam inaweza kuhifadhi programu 4.(0~3)
Hebu tuzime umeme na kupakua programu kwa kutumia "LOAD".
LOAD0 Loaded 30byte OK
Hakiki kwa kutumia "LIST"! Tekeleza kwa kutumia "RUN"!
Kuhakiki programu iliyotunzwa, tumia "FILES".
FILES
Kuwa makini usije ukafuta programu uipendayo kwa makosa.
Kutengeneza programu mpya, tumia "NEW".
NEW OK LIST OK
Kama utachapa "LIST", hakuna chochote kitakachoonyeshwa.
Programu iliyotunzwa katika namba 0 itaanza otomatiki endapo utawasha swichi wakati umeshikilia kitufe cha IchigoJam.
(Hata kama IchigoJam itatenganishwa na kibodi au scrini, itaweza kutumika kwa operesheni za kielektroniki n.k.)
Jaribu sasa!
1. Hebu tunza programu ambayo itawasha mara 3
2. Hebu fanya ianze otomatiki
3. Angalia nini kitatokea endapo utatumia "SAVE" baada ya "NEW"
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp