Tengeneza saa ya kupima wakati / TICK

1,2,3,4,5,6...
mara 60 kama ni sekunde 1, itaendelea kuhesabu muda, IchigoJam.
?TICK()
"TICK" ni hiyo namba. Hebu tufanye ionyeshe mara kadhaa.
?TICK()
Namba iliyoonyeshwa kwa mara ya pili ni kubwa kuliko mara ya kwanza.
?TICK()/60
Kwa kugawanya kwa 60, itabadili muda tokea ulipowasha kuwa katika mfumo wa sekunde.
Tumia komandi "CLT" (kifuta wakati), kuweka upya (reset) namba ambayo inahesabu.
CLT OK ?TICK()/60
Unaweza kufahamu muda tangu kuwekwa upya (reset).
Saa ya kupima wakati ambayo inapima muda kwa sekunde tangu ilipoanzishwa komandi ya "RUN" hadi kitakapobonyezwa kitufe cha IchigoJam.
10 CLT 20 IF BTN()=0 GOTO 20 30 ?TICK()/60
Imekuwa ikisubiri kwa kurudiarudia mpaka ambapo kitufe kilibonyezwa katika mstari wa 20.
Kutengeneza saa ya kupima wakati ambayo itaonyesha muda kila mara utakapobonyeza kitufe.
40 IF BTN()=1 GOTO 40 50 GOTO 10
Jaribu sasa!
1. Hebu vuta pumzi kubwa, na pima ni sekunde ngapi unaweza kutweta kwa ajili ya pumzi.
2. Hebu funga macho, na bonyeza kitufe ili kupata tofauti ya sekunde 5.
3. Hebu tufute "/ 60" katika mstari wa 30 na pima kasi yako mwenyewe ya kubonyeza kitufe tena na tena.
4. Tunza kwa "SAVE0", zima, washa wakati umeshikilia kitufe, kama ilianza otomatiki, hebu bonyeza tena na tena!
5. Hebu tengeneza upya ili ianze kwa kubonyeza kitufe, na kuonyesha kwa kubonyeza kitufe kwa mara ya pili.
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp