Dhibiti muda / WAIT

Hebu tufanye "wait" katika IchigoJam.
Kielekezi cha mraba kinachopepesa katika skrini kina maana kuwa kibodi iko tayari kutumika.
WAIT60
Je umeona kuwa kielekezi kimepotea kwa muda mfupi? Hebu tujaribu tena.
Kama utabadili namba iliyo mbele ya "WAIT", urefu wa muda katika "wait" utaweza kubadilika.
※1 second = 60
WAIT120
Kielekezi kimepotea kwa muda mrefu zaidi kulinganisha na mwanzo.
Kuwasha LED, na kuzima otomatiki.
LED1:WAIT120:LED0
Tumia alama ya nukta mbili ':'(ni rahisi kuichanganya na ya nuktamkato ';') kuunganisha komandi.
Washa kwa "LED1", subiri kwa "WAIT120", zima kwa "LED0".
Kuwasha LED kidogo.
LED1:WAIT3:LED0
Kama utabadili namba kwa ajili ya "WAIT", itabadili muda wa uwakaji wa LED.
Washa LED mara mbili.
LED1:WAIT3:LED0:WAIT3:LED1:WAIT3:LED0
Unaweza kuunganisha zaidi na zaidi kwa kutumia alama ya nukta mbili ":".
Jaribu sasa!
1. Hebu tufanye "WAIT" kwa sekunde 10
2. Washa LED kwa sekunde 5 na kuizima
3. Hebu tufanye "WAIT 10000", kuikatisha katikati tumia kibonye ESCAPE
4. Washa kwa muda mrefu na washa kidogo
5. Hebu jaribu kutengeneza mwanga wa LED katika ruwaza ya kuvutia
CC BY IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp