Tengeneza sauti / BEEP

Hakikisha miguu ya saketi ya sauti imechomekwa katika SOUND(SND) na GND kwenye IchigoJam yako.
BEEP
Je umesikia mlio wa sauti beep?
Toni ya juu.
BEEP 5
Toni ya chini.
BEEP 20
Toni ndefu.
BEEP 10,30
Hebu tutengeneze mdundo!
10 BEEP 5:WAIT 30 20 BEEP 20:WAIT 30 30 GOTO 10 RUN
WAIT ni komandi ya kusubiri. Mdundo wa taratibu utatokea kama utaweka namba kubwa zaidi. GOTO ni komandi ya kurudi nyuma katika mstari wa 10 ili kurudia. Bonyeza kibonye [ESC] kusimamisha.
Mdundo utasimama wakati ukibonyeza kitufe cha IchigoJam yako.
15 IF BTN() GOTO 15
Hebu Jaribu!
1. Tengeneza sauti mbalimbali!
2. Tengeneza mdundo wenye tempo ya kasi (fast tempo)
3. Ongeza programu hii "12 BEEP 20:WAIT 30" ili kubadili iwe tripple time (musical time pattern)
4. Ifanye ya mdundo wa quadruple
5. Badili mdundo "GOTO 15" kuwa "GOTO 10" katika mstari wa 15
6. Tengeneza mdundo wako asili!
CC BY on GitHub IchigoJam print https://ichigojam.github.io/print/sw/ IchigoJam®jig.jp